UbongoUbongoUbongoUbongo
  • Home
  • What we do
    • What we do
    • How we do it
    • Where we work
    • Meet the team
    • Building Brains Conference
  • Impact
    • Impact
    • Annual Report
    • Research Studies
    • Roadshows
  • Partnerships
    • Partnerships
    • Case Studies
    • Partners Portfolio
  • Shows
    • Shows
    • Nuzo and Namia
    • Akili and Me
    • Ubongo Kids
    • Akili Family
    • TV Showtimes
    • Radio Showtimes
    • Listen/Chat on Mobile
  • Blog
    • Blog
    • Photo Gallery
    • Video Gallery
    • Infographic Gallery
  • Contact
  • Donate

Mbinu TANO za kumwezesha mwanao afanye vizuri shuleni!

    Home Blog Mbinu TANO za kumwezesha mwanao afanye vizuri shuleni!
    NextPrevious

    Mbinu TANO za kumwezesha mwanao afanye vizuri shuleni!

    By ubongo | Blog, Ubongo, Ubongo Kids | Comments are Closed | 9 January, 2017 | 2

    Wakati umewadia! Shule zimefunguliwa! 

    Twajua una malengo makubwa kwa ajili ya mwanao. Unataka ang’are! Afanye vizuri. Afanikiwe! Hivyo basi, tumekuandalia mbinu hizi TANO zitakazomsaidia mtoto wako afanikiwe si tu shuleni, bali pia katika kila afanyacho!

     1. Soma naye!

    Keti na mwanao msome pamoja! Someni vitabu, pitieni magazeti, zungumzeni! Mwulize maswali kuhusu mnachosoma. Kusoma mara kwa mara humpa mtoto msingi imara wa LUGHA, utakaofanya awe na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha na kufanya watu wamuelewa katika chochote atakachofanya maishani. Kusoma pamoja kutafanya pia uwe karibu na mwanao!

     

     

    2. Huko shule anafanya nini?

    Kila anapotoka shule, piga naye stori! Mwulize siku yake imeendaje, na amejifunza nini. Usiulize tu alichofanya, bali mwambie AKUELEZEE hicho alichosoma siku hiyo!  Hii ni mbinu nzuri ya kuhakikisha anafanya marudio, na hukuonyesha pia maeneo ambayo anahitaji msaada!

     

    3. Zungumza na mwalimu wake kila mara!

    Ongea na walimu wake mara kwa mara! Fahamu maendeleo ya mwanao! Je, anafanya vizuri kama mwalimu wake anavyotaka? Anahitaji msaada? Keti na mwalimu mpange mikakati ya kumsaidia mtoto wako afanye vizuri shuleni!

     

    4. Fahamu anachopenda!

    Mwanao anapenda hesabu? Ana shauku ya kujifunza zaidi Kiswahili, ama Kiingereza, au kuchora? Mtie moyo kila anapofanya mazoezi ya masomo haya. Lakini pia usisahau kutazama maeneo mengine anapohitaji msaada zaidi!

     

    5. Mfanye apende kujifunza!

    Tengeneza mazingira yanayofanya mtoto wako afurahie kujifunza, hasa pale anapotoka shule. Cheza naye michezo mbali mbali! Undeni vitu pamoja! Tumieni teknolojia kujifunza! Fanya yale  yanayomsukuma mwanao atumie #akili!

     


    Mpatie mwanao msingi IMARA wa ELIMU kwa kutumia app zetu za BURE, zinazopatikana kwa KIINGEREZA na KISWAHILI. Zitamwezesha ajifunze herufi na maneno mapya katika mazingira yanayomfurahisha na kumburudisha!

    Afrika, Akili and Me, back to school, Kiingereza, kiswahili, mwalimu, shule, soma, soma naye, Tanzania, twaenda shule, Ubongo, Ubongo kids

    NextPrevious

    Categories

    • Akili and Me
    • Akili Family
    • Akili Radio
    • Blog
    • Caregivers
    • Covid-19
    • Digital
    • Francophone
    • Infographic
    • Kenya
    • Last Mile
    • Malawi
    • Neurodiversity
    • Nigeria
    • Nuzo and Namia
    • Partners
    • PlayMatters
    • Press
    • Rwanda
    • South Africa
    • Tanzania
    • Toolkits
    • Ubongo
    • Ubongo Impact
    • Ubongo Kids
    • Ubongo Kids Club
    • Ubongo Mobile
    • Ubongo Videos
    • Ubongoers
    • Uganda
    • Uncategorized
    • Utu
    • Utu Clubs
    • Video
    Ubongo Logo

    Ubongo is Africa's leading producer of kids' edutainment. As a non-profit social enterprise we create fun, localised and multi-platform educational content that helps kids learn, and leverage their learning to change their lives. We reach millions of families across Africa through accessible technologies like TV, radio and mobile phones.

    LATEST NEWS

    • 12 April, 2025
      0

      COSOTA MAGAZINE – VIRTUAL VERSION: Jrida la Mtandaoni la COSOTA

    • 9 April, 2025
      0

      Akili and Me Hits 1 Million YouTube Subscribers!

    LINKS

    • Home
    • What we do
    • Impact
    • Partnerships
    • Shows
    • Blog
    • Newsletter
    • Contact
    • Donate
    • Careers
    • Privacy Policy
    • Terms and Conditions
    • Cookie Policy
    • Sitemap
    • Annual Report

    CONTACT US

    General inquiries:
    info@ubongo.org

    Marketing and merchandising:
    marketing@ubongo.org

    Partnerships and donation:
    partnerships@ubongo.org

    Phone: +255 685 012 897

    • EN
    • SW
    • FR
    • EN
    • SW
    • EN
    • Home
    • What we do
      • What we do
      • How we do it
      • Where we work
      • Meet the team
      • Building Brains Conference
    • Impact
      • Impact
      • Annual Report
      • Research Studies
      • Roadshows
    • Partnerships
      • Partnerships
      • Case Studies
      • Partners Portfolio
    • Shows
      • Shows
      • Nuzo and Namia
      • Akili and Me
      • Ubongo Kids
      • Akili Family
      • TV Showtimes
      • Radio Showtimes
      • Listen/Chat on Mobile
    • Blog
      • Blog
      • Photo Gallery
      • Video Gallery
      • Infographic Gallery
    • Contact
    • Donate
    Ubongo